Iran imesema Jumapili kuwa itafanya mazungumzo ya nyuklia katika siku zijazo na nchi tatu za Ulaya ambazo zilianzisha azimio la kupinga azimio dhiai yake lililopitishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti silaha za atomiki.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran, Esmaeil Baghaei amesema mkutano wa manaibu mawaziri wa mambo ya nje wa Iran, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza utafanyika siku ya Ijumaa bila ya kutaja eneo la mkutano.
Masuala mbalimbali ya kikanda na kimataifa na mada, ikijumuisha masuala ya Palestina na Lebanon, pamoja na suala la nyuklia yatajadiliwa, msemaji huyo alisema katika taarifa ya wizara ya mambo ya nje.
Baghaei ameuelezea mkutano huo kama mwendelezo wa mazungumzo ya Septemba, na nchi hizo katika mikutano inayofanyika pembeni mwa mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York nchini Marekani.