Hata hivyo, umoja huo umesema kwamba hauwezi kutaja jeshi la kulinda mapinduzi ya Iran kuwa kundi la kigaidi bila ya kuwepo maamuzi ya mahakama.
Uhusiano kati ya Umoja wa ulaya wenye wanachama 27 na Iran, uliharibika baada ya kuvunjika kwa mazungumzo kuhusu mpango wake wa Nyuklia, na Iran kuwakamata raia kadhaa kutoka nchi za Ulaya.
Umoja wa ulaya umekuwa ukikosoa msako wa maafisa wa usalama wa Iran dhidi ya waandamanaji, ikiwemo kuwanyonga waandamanaji na kutoa msaada wa ndege zisizo na rubani kwa Russia katika vita vyake nchini Ukraine.
Miongozi mwa vikwazo vipya vya umoja dhidi ya Iran, vinalenga waosimamia na kuendelea oparesheni dhidi ya waandamanaji.