Iran iliamuru uchunguzi ufanyike kuhusu video na picha za ghasia za vikosi vya serikali

Watu wanapeperusha bendera za Iran za kabla ya mapinduzi ya Kiislamu waliposhiriki katika maandamano dhidi ya mamlaka ya Irani, mjini London, Jumamosi, Oktoba 29, 2022. (AP)

Iran iliamuru uchunguzi ufanyike siku ya Jumatano kuhusu video na picha za ghasia za vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya waandamanaji wa Iran.

Katika mojawapo ya video hizi, maaskari kadhaa wa serikali wanaonekana wakimpiga mwanamume mmoja vibaya sana. Kisha mmoja wa mawakala hao anamgonga mtu huyo na pikipiki na wakala mwingine anampiga risasi kutoka karibu. Uhalisia wa picha hizi, kama video nyingine nyingi zilizotolewa kutokana na maandamano yanayoendelea nchini Iran, hauwezi kuthibitishwa bila kushikamana na upande wowote.

Video hiyo ilionekana kwenye mitandao ya kijamii Jumanne jioni na inadaiwa kutoka Tehran.

"Video hii ya kushtua iliyotumwa kutoka Tehran leo ni ukumbusho mwingine wa kutisha kwamba ukatili wa vikosi vya usalama vya Iran hauna kikomo. Katikati ya mzozo wa kushambulia watu bila kufunguliwa mashitaka wamepewa uhuru wa kuwapiga kikatili na kuwapiga risasi waandamanaji," Amnesty International ilisema kupitia Twitter.