Lakini ameeleza kuwa kama Marekani inaendeleza vitisho na vikwazo, basi Iran haraka itaweza kurejea kwenye harakati zake za nyuklia hadi kufikia kiwango cha juu kabla ya mkataba kuanza kazi.
Akizungumza na wabunge kwenye hotuba iliyotangazwa na televisheni, Rouhani alisema Marekani si mshirika mzuri.
“Wale ambao wanajaribu kurudi kwenye lugha za vitisho na vikwazo ni wafungwa wa mitazamo yao ya nyuma,” Rouhani alisema. wanajinyima fursa ya amani.
Iran inapinga vikwazo vipya, ambavyo rais wa Marekani Donald trump alitia saini mwanzoni mwa mwezi huu dhidi ya watu waliohusika na program ya makombora ya masafa marefu ya iran na kikosi maalum cha ulinzi cha Revolutionary Guard.
Hatua hiyo ya Trump imekuja ikiwa ni ujumbe wa kuitaka Iran isiendelee na majaribio ya makombora ya masafa ya marefu.