Wito huo unatolea baada ya Pakistan kuamuru siku ya Jumanne wahamiaji wote waishio nchini humo kinyume cha sheria, wakiwemo raia milioni 1.7 wa Afghanistan, kuondoka ifikapo tarehe 1 Novemba au wafukuzwe na kurejeshwa nchini mwao.
Familia nyingi tayari zimeondoka kwenda Afghanistan ili kuepuka kukamatwa na kufukuzwa kwa nguvu, huku wizara ya habari ya Pakistan ikitoa taarifa ya kila siku kwa wale wanaohusika na sera hiyo kwamba siku zao za kukaa nchini humo zinakaribia kumalizika.
“Afghanistan inapitia mzozo mbaya wa kibinadamu pamoja na changamoto kadhaa za haki za binadamu, hasa kwa wanawake na wasichana, imesema taarifa ya pamoja ya shirika la kimataifa la uhamiaji na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.