IOC kufanya uchaguzi wa mkuu wake mpya

Wagombea saba watashindania moja ya kazi kubwa na bora zaidi katika ulimwengu wa michezo ambayo kawaida hugombaniwa kila baada ya miaka 12.

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Jumatatu imetangaza wanachama wake katika klabu ya kipekee na yenye kuhitaji busara kubwa, wamejitosa katika kinyang’anyiro cha kuwa rais wake ajaye wa kamati hiyo.

Uchaguzi wa kura ya siri utafanyika mwezi Machi. Mshindi atachukua nafasi ya Thomas Bach, wakili wa Ujerumani ambaye atajiuzulu mwezi Juni baada ya kufikisha miaka 12 akiwa madarakani.

Rais wa 10 wa IOC anaweza kuwa kwa mara ya kwanza mwanamke, kutoka Afrika au Asia, au hata kutoka Uingereza kwa mara ya kwanza.

Watachukua usimamizi wa shirika thabiti la kifedha ambalo linahitaji ujuzi wa kitaalamu katika nyanja zenye changamoto za michezo na siasa za kikanda na ulimwengu.