Serikali ya India imepinga kutambuliwa kwa ndoa za jinsia moja ikiwa ni kujibu maombi yaliyowasilishwa katika Mahakama ya Juu.
Lakini walio fungua shauri na wanaharakati wa haki za mashoga bado wana matumaini ya kupata haki hiyo kwa jumuiya yao.
Ikiliita suala la “umuhimu mkubwa” mahakama iliunda jopo la majaji watano Jumatatu ili kusikiliza hoja za mwisho kuanzia Aprili 18.
Serikali inayoongozwa na chama cha Hindu Bharatiya Janata imeiambia mahakama kwamba ndoa ya watu wa jinsia moja haiendani na maana kamili ya familia za Wahindi, na inapaswa kuachiwa bunge kufanya mabadiliko yoyote katika sheria za ndoa.
Mahakama haiwezi kutakiwa kubadilisha sera nzima ya kutunga sheria ya nchi iliyoingia kwa kina katika kanuni za kidini na kijamii,” ilisema.