India inatarajiwa kutuma chombo cha utafiti kwenye mwezi, leo Ijumaa.
Iwapo chombo hicho kitafanikiwa, itakuwa mara ya nne kwa India kufanya hivyo baada ya Marekani, Umoja wa Sovieti na China.
Itachukua muda wa mwezi mmoja kwa chombo hicho kwa jina Chandrayaan, ambacho kimegharimu dola milioni 75, kufika sehemu ya kusini mwa mwezi.
Chombo hicho kitafika Agosti.
Sehemu ya mwezi ambacho chombo hicho kinakwenda, imewavutia wanasayansi kwa sababu wanaamini kwamba sehemu hiyo ina maji.