India inaondoa raia wake Cambodia walioshirikishwa na njama za udanganyifu

Ramani ya Cambodia. (Courtesy of Google)

Ubalozi wa India nchini Cambodia unafanya kazi na mamlaka za Cambodia na umewaokoa na kuwarudisha nyumbani takriban raia wa India 250

Serikali ya India imesema inawaondoa raia wake ambao walishawishiwa kuingia katika ajira nchini Cambodia na walilazimishwa kushiriki katika njama za udanganyifu wa mtandaoni.

Ubalozi wa India nchini Cambodia unafanya kazi na mamlaka za Cambodia na umewaokoa na kuwarudisha nyumbani takriban raia wa India 250, ikijumuisha raia 75 katika miezi mitatu iliyopita, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa India, Randhir Jaiswal amesema katika taarifa siku ya Jumamosi.

Jaiswal alikuwa akijibu ripoti za habari za India ambazo zilisema zaidi ya raia wa India 5,000 wamekwama nchini Cambodia na kulazimishwa kufanya udanganyifu wa kimtandao kwa watu kwenye nchi yao.

Tunafanya kazi pia na mamlaka za Cambodia pamoja na mashirika nchini India ili kuwakamata wale waliohusika na mipango hii ya udanganyifu, Jaiswal alisema.