IMF yatoa wito kwa mataifa ya Kiafrika kuandaa miradi inayoweza kupata ufadhili

Your browser doesn’t support HTML5

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Fedha, IMF, Kristalina Georgieva yuko nchini Rwanda kwa ziara ya siku tatu. Akiwa mjini Kigali amekutana na mawaziri wa fedha pamoja na magavana wa benki kuu za Rwanda, Uganda, Kenya na Sudan Kusini.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kwamba shirika lake liko tayari kusaidia miradi mikubwa ya maendeleo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Amesema ili mataifa haya yaweze kufanikiwa kuna umuhimu wa kuandaa miradi mizuri ambayo inaweza kupata ufadhili hasa kwa kuzingatia kuwa pesa iliyopo haitoshi.