IMF imetoa wito wa utekelezaji wa makubaliano ya deni la Zambia

Mkurugenzi mtendaji wa IMF, Kristalina Georgieva

Zambia ambayo deni lake la jumla ni dola bilioni 32.8, ilishindwa kulipa  deni lake la nje la dola bilioni 18.6 mwaka 2020 wakati wa janga la Covid.

Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) limetoa wito wa utekelezaji kwa muda unaostahili wa makubaliano ya deni la Zambia wakati ikitoa dola milioni 189, ikiwa ni sehemu ya mpango wa msaada wa dola bilioni 1.3 kwa taifa hilo lenye utajiri wa shaba.

Zambia, ambayo deni lake la jumla ni dola bilioni 32.8, ilishindwa kulipa deni lake la nje la dola bilioni 18.6 mwaka 2020 wakati wa janga la Covid. Wakopeshaji wake wa kigeni walikubaliana kurekebisha karibu theluthi moja ya deni la nchi hiyo mwezi uliopita, kufuatia miaka miwili ya mashauriano magumu.

Kristalina Georgieva, mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, alitoa wito wa “utekelezaji kwa wakati wa makubaliano haya.”