IGAD kuanza mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir

Wafungwa walioachiwa ni pamoja na Pagan Amum, katibu mkuu wa zamani wa chama tawala cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM), Majak D’Agot, Oyai Deng Ajak na Ezekiel Lol Gatkuot
Serikali ya Sudan Kusini inatarajia kufikia hatua za kimaendeleo katika mashauriano ya amani na waasi, kufuatia kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa walioshukiwa kupanga njama za kuiangusha serikali ya Rais Salva Kiir, kwa mujibu wa msemaji wa Rais, Ateny Wek Ateny.

Duru ijayo ya mazungumzo ya nchi za jumuiya ya IGAD inayofadhili mazungumzo ya amani yanayofanyika katika nchi jirani ya Ethiopia imepangwa kuanza leo Jumatatu katika mji mkuu Addis Ababa.

Wafungwa walioachiwa ni pamoja na Pagan Amum, katibu mkuu wa zamani wa chama tawala cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM), Majak D’Agot, Oyai Deng Ajak na Ezekiel Lol Gatkuoth.

Kuachiwa kwa wafungwa hao kumekuwa moja ya dai kubwa kutoka kwa wawakilishi wa waasi waliopo kwenye mashauriano ya amani, ambao wanamuunga mkono makamu rais wa zamani Riek Machar.