IEBC yaomba ufafanuzi Mahakama ya Juu

Maafisa waandamizi wa tume ya uchaguzio na mipaka ya Kenya, IEBC, wakizungumza na waandisha wa habari mjini Nairobi, Kenya.

IEBC imewasilisha hoja kwenye Mahakama ya Juu nchini Kenya kutaka ufafanuzi juu ya marudio ya uchaguzi wa Octoba 26.

Huku mapendekezo mapya kuhusu sheria za uchaguzi nchini Kenya yakiendelea kuibua hisia mbali mbali, siku ya Alhamisi mwenyekikti wa tume ya uchaguzi na mipaka, IEBC, Wafula Chebukati, aliwasilisha hoja kwenye mahakama hiyo.

IEBC inataka ufafanuzi wa sehemu moja ya uamuzi wake kuhusu utaratibu unaotakiwa kufuatwa katika uchaguzi wa marudio.

Chebukati anataka kujua majukumu yake kuhusu kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi baada ya mahakama ya juu kutoa uamuzi ambao, anasema, umeleta mkanganyiko.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA amezungumza na wakili Kamau Mbugua, ambaye ni mchambuzi wa masuala ya siasa, na akaanza kwa kumuuliza kuelezea ni nini kimechangia IEBC kuchukua hatua hiyo.

Your browser doesn’t support HTML5

Mwenyekiti wa Tume ya IEBC kenya apeleka hoja mahakamani

Imetayarishwa na Mwandishi wetu BMJ Mriithi, Washington, DC.