Katika taarifa kwa waandishi wa ghabari. Chebukati alisema ametumia kipengele cha 138 cha katiba ya Kenya kufanya uteuzi huo.
Hayo yanafuatia kauli ya Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, kwamba muungano wa upinzani, NASA, hautashiriki katika uchaguzi huo wa marudio, iwapo hakuna "hakikisho la kisheria na kikatiba kwamba uchaguzi huo wa huo utakuwa huru na wa haki."
Odinga, ambaye aligombea urais mapema mwezi jana kwa tikiti ya muungano wa upinzani, NASA, ametoa shinikizo kwamba ni sharti maafisa sita wa tume ya uchaguzi na mipaka, IEBC, waondolewe kabla ya uchaguzi huo kufanyika.
Tume ya IEBC ilitangaza tarehe 17 Oktoba kama siku ya uchaguzi huo wa urais, baada ya mahakama ya juu kubatilisha uchaguzi uliompa ushindi rais Uhuruu Kenyatta katika uamuzi uliotolewa siku ya Ijumaa.
Upinzani unashikilia kwamba tume hiyo imegubikwa na dosari na haiwezi kusimamia uchaguzi huo kabla ya kufanyiwa mabadiliko. Wanasiasa wa chama kinachotawala cha Jubilee wanmesema kuwa wako tayari kushiriki kwenye uchaguzi huo.
Katika uteuzi huo wa IEBC, nafasi ya afisa mkuu wa kusimamia uchaguzi huo imechukuliwa na Marjan Hussein Marjan, ambaye alikuwa naibu wake afisa mkuu anayekabiliwa na tuhuma za dosari, Ezra Chiloba.
Shughuli za upigaji kura zitasimamiwa na Dkt Sidney Namulungu huku masuala ya mikakati ya tume hiyo yakisimamiwa na Bi Nancy Kariuki.
Idara ya mawasiliano na teknolojia, iliyosimamiwa na marehemu Chris Msado, sasa itasimamiwa na Albert Gogo.
Bernard Misati Moseti ndiye atakayesimamia mafunzo ya maafisa wa IEBC huku Silas Rotich akisimamia kituo cha kitaifa cha kuratibu masuala ya upigaji kura na kutangaza matokeo ya kura ya urais.