Idriss Deby Itno rais aliyekaa muda mrefu madarakani

Aliyekuwa rais wa Chad hayati Idriss Deby Itno.

Hapo Desemba 1, 1990, raia wa chad walishuhudia kiongozi mwembamba wa kijeshi akijitokeza kwenye televisheni, dhahiri akionekana ana wasi wasi kidogo. Idriss Deby Itno, mshirika wa zamani wa karibu wa Rais Hissene Habre, ambaye alimuasi, na kukamata madaraka baada ya wanajeshi wake kuingia katika mji mkuu N’Djamena. Aliacha mavazi yake ya kijeshi kwa kuivaa siasa, na hapo Desemba 4, alikuwa rais wa Baraza la Serikali.

In 1996,Mwaka 1996, baada ya ‘kipindi cha mpito cha kidemokrasia’ Deby alichaguliwa rais katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na aliwateua baadhi. Ya wapinzani katika serikali. Mwaka 2003, Chad ilikuwa nchi inayozalisha mafuta. Ilichukua fursa ya hali nzuri katika sekta ya mafuta, Idriss Deby aliwekeza kwa kiasi kikubwa sana katika jeshi kwa kununua vifaa vingi. Alikuwa na jukumu kuu katika siasa za kieneo kwa kupeleka wanajeshi wa Chad katika tume za amani na operesheni dhidi ya ugaidi.

Idriss Deby Itno alichaguiwa tena kila mara lakini alilazimika kukabiliana na makundi ya uasi. Mwaka 2009, waasi hata walifanikiwa kuingia katika mji mkuu, lakini hawakuweza kuzimwa shukran kwa uingiliaji kati wa Ufaransa. Kama kiongozi wa jeshi, Rais Idriss Deby Itno mara kwa mara alikwenda mstari wa mbele. Alipandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Jeshi la Chad hapo Agosti 11, mwaka 2020, katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Chad.

Uasi ulizuka April 11, mwaka 2021, siku ya uchaguzi, wakati Rais wa Chad alipokuwa anawania awamu ya sita ya uongozi. Kwa mara nyingine tena alikwenda mstari wa mbele ambako alijeruhiwa na baadaye kuchukuliwa kwenda mjini. Alishindwa kuhimili majeraha aliyoyapata, siku hiyo baada ya tangazo la ushindi wake katika uchaguzi akiwa amepata karibu asilimia 79 ya kura.