Mgombea wa mrengo wa kulia Calin Georgescu aliongoza wagombea wegine wote kwa karibu asilimia 23 ya kura, licha ya kuwa hakufikisha hata asilimia kumi kwenye kura ya maoni kabla ya uchaguzi. Georgescu Desemba 8 atashindana kwenye kura ya marudio na Elena Lasconi wa mrengo wa kati kulia ambaye alikuwa kwenye nafasi ya pili kwa asilimia 19, akitarajia kupata uungaji mkono kutoka kwa vyama vilivyoshindwa vya kushoto na kati.
Uchaguzi wa bunge wa taifa hilo pia itafanyika Desemba mosi. Baraza Kuu la Usalama linaloongzwa na rais wa sasa Klaus lohannis linakutana leo Alhamisi ili kutadhimi uwezekano wa tishio la usalama wa kitaifa uliopelekewa na vitendo vya kimitandao , kulingana na taarifa iliotolewa Jumatano na ofisi ya rais.
Wakati huo huo baraza la kitaifa la habari la Romania ambalo linaratibu utangazaji na mitandao ya kijamii limeomba Kamisheni ya Ulaya ichunguze jukumu la Tik Tok kwenye uchaguzi wa Jumapili, wakati kukiwa na tetesi kuwa huenda jukwaa hilo lilishinikiza maoni ya umma, kulingana na shirika la habari la Reuters.