Operesheni kubwa ya kuwatafuta manusura ilikuwa ikiendelea karibu na mji wa pwani wa Malindi ambako miili kadhaa ilifukuliwa mwishoni mwa jumaa, hali iliyozua taharuki nchini Kenya, huku Rais William Ruto akiapa kukabiliana na mienendo ya kidini “isiyokubalika.
Uchunguzi ulianzishwa dhidi ya kanisa la Good News International Church na kiongozi wake Paul Mackenzie Nthenge ambaye alitajwa katika hati za mahakama, ambaye alihubiri kuwa kifo cha njaa kitawafikisha waumini kwa Mungu.
Inaaminika kuwa baadhi ya waumini wake bado wanajificha msituni karibu na kijiji cha Shakahola, ambao ulivamiwa na polisi mapema mwezi huu baada ya taarifa kutoka kwa kundi la eneo hilo linalofanya kazi bila kutafuta faida.
“Tulipata miili 73 kutoka msituni kufikia jioni na zoezi litaendelea Jumanne,” afisa wa polisi anehusika katika uchunguzi ambaye hatuka jina lake litajwe ameiambia AFP. Utapata mengi Zaidi katika ripoti za waandishi wetu, baadaye kwenye matangazo hayo.