Mauaji hayo yametokea wakati ambapo maelfu wakiwa wamekusanyika Jumatatu kupinga maandalizi ya Marekani kuhamisha rasmi ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.
Maafisa wa afya wamesema sio chini ya watu 500 wamejeruhiwa, wakiwemo dazeni ya wale waliojeruhiwa kwa risasi.
Vifo vinafanya idadi ya Wapalestina waliouwawa na majeshi ya Israeli katika wiki sita za maandamano kufikia kiasi cha watu 50.
Wakosoaji wa mauaji hayo wameyalaumu majeshi ya Israeli kwa kutumia risasi za moto, wakati Israeli ikisema hatua iliochukuwa ni muhimu kwa usalama kwani watu walio kusanyika walikuwa ni tishio kwenye usizio mpakani hapo.
Zaidi ya hapo kumekuwa na utupaji wa risasi upya Jumatatu kutoka upande wa Israeli.
Majeshi hayo ya ulinzi yalitupa upande wa waandamanaji mabomu ya machozi, lakini makundi hayo ya watu yalionekana kutoweza kudhibitiwa na yalionekana kuendelea kukusanyika eneo hilo.