Shirika la kimataifa la uhamiaji Jumapili limeongeza makadirio yake ya idadi ya vifo kutoka kwa maporomoko makubwa ya ardhi huko Papua New Guinea, na kufikia zaidi ya 670.
Serhan Aktoprak, mkuu wa ujumbe wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa katika taifa hilo la visiwa vya Pasifiki Kusini, amesema idadi iliyorekebishwa ya waliofariki ilitokana na hesabu zilizofanywa na maafisa wa kijiji cha Yambali na jimbo la Enga kwamba zaidi ya nyumba 150 zilifukiwa na maporomoko ya udongo yaliyotokea Ijumaa.
Makadirio ya awali yalikuwa ni nyumba 60.
Maafisa wa eneo hilo hapo awali walikuwa wameweka idadi ya vifo siku ya Ijumaa kuwa 100 au zaidi. Maiti watano pekee na mguu wa muathirika wa sita ulipatikana siku Jumapili.