Idadi ya uambukizaji wa VVU yapunguka Tanzania

Ufukara ni sababu moja kuu ya ikuenea kwa Ukimwi katika nchi nyingi za afrika

Wakati dunia inaadhimisha siku ya Ukimwi Duniani, takwimu za kitaifa nchini Tanzania za mwaka 2012 zinaonyesha maambukizi ya ugonjwa huo yamepungua kutoka asilimia 9.2 mpaka asilimia 5.1 hivi sasa.

Kwa mujibu wa Takwimu hizo katika maeneo ya mijini maambukizi ya ukimwi yako juu kwa asilimia 7.2 wakati kwa maeneo ya vijijini ni asilimia 4.3 ya maambukizi, ambapo wanaume walioambukizwa ni asilimia 3.8.,huku wanawake wenye VVU wakifikia asilimia 6.2

Viongozi mbalimbali nchini Tanznaia akiwemo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete wamekuwa wakihimiza watanzania kujitokeza kupima virusi vya ukimwi kwa hiari kama moja ya njia ya kupunguza maambukizi mapya ya ukimwi.

Your browser doesn’t support HTML5

Idadi ya uambukizaji wa VVU yapungua Tanzania


Katika tamko rasmi la serikali ya Tanzania juu ya siku ya ukimwi duniani kwa mwaka huu wa 2013, waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi alizungumzia kauli mbiu ya siku ya ukimwi duniani hapa nchini kwa mwaka huu.

Nchini Tanzania kumefanyika maonyesho maalum ya mashirika na taasisi mbali mbali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi nchini....lengo likiwa ni kutoa hamasa kwa jamii kushirika mapambano dhidi ya ukimwi ambapo viongozi mbalimbali wa serikali wamesisitiza kwamba pamoja na wananchi wengi kuelewa njia mbali mbali za kuenea kwa ugonjwa huo bado zinahitajika juhudi katika kuhakikisha hakuna maabukizi mapya.

Aidha akizungumzia malengo ya 000, ya maambukizi ya virusi vya ukimwi Mwenyekiti wa Mtandao wa kupunguza matumizi ya dawa za kulevya Tanzania, Godfrey Teri amesema kuwa makundi maalum hayana budi kushirikishwa katika mapambano dhidi ya ukimwi wakiwemo watumiaji wa dawa za kulevy

Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na kutumia dawa za kufubaza virusi ARVS nao walizungumzia changamoto ambazo bado wanakabiliana nazo ikwemo kutopatikana kwa wingi dawa hizo kama anavyozungumza Mwanahamis Mhando kutoka mtandao wa wanaoishi na virusi vya ukimwi Tanzanai TACOPHA.

Unyanyapaa na kutojikubali wanaojikuta wameambukizwa virusi vya ukimwi navyo bado ni changamoto kubwa kwa jamii nchini Tanzania lakini hata hivyo Said Kambangwa ambaye pia anatoka Baraza la wanaoishi na virusi vya Ukimwi TACOPHA amesema namna bora ya kukabiliana navyo ni elimu na ushauri nasaha

Matokeo ya utafiti wa viashiria vya VVU na Ukimwi Tanzania mwaka 2011/2012 unaonyesha kuwa ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya ukimwi umeongezeka kwa kiasi kikubwa ambapo hivi sasa asilimia 62 ya wanawake na asilimia 47 ya wanaume kati ya miaka 15 na 49 wamewahi kupima VVU na kupokea majibu yao ukilinganisha na asilimia 37 tu ya wanawake na 27 ya wanaume mwaka 2007 - 2008.