ICC imesema iligundua shughuli isiyo ya kawaida kwenye mtandao wa kompyuta zake mwishoni mwa wiki iliyopita, na inaendelea kushughulikia tatizo hilo.
Msemaji wa mahakama hiyo amekataa kutoa maelezo juu ya ukubwa wa udukuzi huo, na iwapo tatizo hilo limemalizika kabisa au nani alifanya udukuzi huo.
“Hatua za haraka zilichukuliwa kukabiliana na tukio hilo la udukuzi wa mtandaoni na kupunguza athari zake,” ICC imesema katika taarifa.
Mahakama hiyo ya uhalifu wa kivita yenye makao yake the Hague Uholanzi, iliundwa mwaka 2002 kushughulikia kesi za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Waendesha mashtaka kwenye mahakama hiyo kwa sasa wanafanya uchunguzi wa kesi 17 kuhusu Ukraine, Uganda, Venezuela, Aghanistan na Ufilipino kati ya nyingine.