Waziri Mkuu wa taifa hilo Viktor Orban, ambaye ameliongoza taifa hilo la Ulaya ya kati tangu 2010, wakati akijitahidi kulifanya kuwa la demokrasia ya kilibelari, licha ya mzozo wa mara kwa mara na Brussels, kuhusu utawala wa kisheria na haki za binadamu.
Orban ndiye kiongozi pekee wa Ulaya aliyedumisha uhusiano na Russia, licha ya uvamizi wa Ukraine. Kufikia sasa amekataa kutuma silaha kwa Kyiv, huku akikosoa vikwazo ilivyowekewa Russia kutokana na vita hivyo. Mwaka jana bunge la Ulaya lilitoa pendekezo likiangazia kuzembea kwa Hungary kwa thamini za demokrasia, wakati likihoji uwezo wake wa kuongoza EU kwa muda wa miezi 6.
Hata hivyo Budapest imesisitiza iko tayari kuongoza Umoja huo wenye mataifa 27 wanachama. ”Tutakuwa wapatanishi wenye haki, kwa ushirikiano wa wanachama wote, pamoja na taasisi,” amesema waziri wa Hungary kwenye maswala ya EU, Janos Boka.