Human Rights Watch yakosoa hukumu aliyopewa mwandishi wa Marekani nchini Mnyanmar

Mwandishi wa Marekani Danny Fenster ahukumiwa miaka 11 jela huko Myanmar

Shirika la kutetea haki za binadam la Human Rights Watch limekosoa hukumu aliyopewa mwandishi habari wa Marekani Danny Fenster  ya kifungo cha miaka 11 jela huko Myanmar

Shirika la kutetea haki za binadam la Human Rights Watch limekosoa hukumu aliyopewa mwandishi habari wa Marekani Danny Fenster ya kifungo cha miaka 11 jela na mahakama moja nchini Mnyanmar inayotawaliwa na wanajeshi.

Mahakama hiyo imetoa hukumun hiyo dhidi ya Fenster, kwa tuhuma za kkukusanyika na watu kinyume cha sharia, uchochezi dhidi ya jeshi, na kukiuka sharia za viza, wakili wake na mwajiri wake walisema leo Ijumaa.

Than Zaw Aung, wakili wa Fenster aliiambia VOA kwa sasa hakuna mipango ya kukata rufaa. Fenster anakabiliwa na mashtaka ya ziada ya uchochezi na ugaidi, ambayo yanaweza kumtia jela maisha.

Wakili wake alisema Jumatano lakini hakuweza kueleza kwa nini mashtaka hayo mapya yaliwekwa, au kile ambacho maafisa wa usalama wanashutumu Fenster amefanya. Mashtaka ya ziada yaliwasilishwa chini ya kifungu cha 124A cha kanuni ya adhabu ya Myanmar, ambayo inakataza uchochezi dhidi ya serikali, na chini ya kifungu cha 50A cha sharia ya kupambana na ugaidi ya Myanmar, ambayo ni uhalifu kwa kuwasiliana na makundi ya ugaidi.