Hukumu ya kifo dhidi ya wanajeshi DRC

Wanajeshi was Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo walipowasili katika mji wa Kibumba ulipoko katika mpaka wake na Rwanda Juni 11, 2014. Picha na REUTERS/Kenny Katombe.

Wanajeshi 23 wanakabiliwa na hukumu ya kifo au kifungo cha kati ya miaka 10 hadi 20 gerezani, baada ya kufikishwa mahakamani jana Jumatatu kwa mashtaka ya kunajisi, kuhepa kazi na makosa mengine jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Hayo yanajiri wakati mapigano yanaendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Wanajeshi hao wamefikishwa katika mahakama ya kijeshi ya Butembo, kivu kaskazini.

Kwa miaka mingi, wanajeshi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamekuwa wakipigana na zaidi ya makundi ya waasi 120 mashariki mwa nchi, ambako kuna utajiri wa madini.

DRC ilirudisha hukumu ya kifo mwezi March mwaka huu, hatua ambayo ilikoselewa na wanaharakati wa haki za kibinadamu.

Mwezi May, wanajeshi wanane walihukumiwa kifo kwa kutoroka mapigano huku wengine wakihukumiwa kifo mwezi July kwa makosa saw ana hayo. Hakuna taarifa iwapo waliohukimwa wameuawa.