Huduma ya afya ya Obamacare nchini Marekani inazidi kupata neema

Huduma ya afya ya bei nafuu Marekani maarufu Obamacare

Huduma ya afya ya bei nafuu Marekani maarufu Obamacare

Mahakama katika uamuzi ilipiga kura saba dhidi ya mbili na kutupilia mbali juhudi za majimbo 18 yanayoongozwa na warepublican na utawala wa Rais wa zamani Donald Trump wa kubadilisha sheria ya huduma ya afya ya bei nafuu ya mwaka 2010 maarufu Obamacare

Mahakama ya juu ya Marekani kwa mara ya tatu ilikataa changamoto kwa sheria kuu ya bima ya afya nchini ambayo inawapa fursa kwa mamilioni ya wamarekani msaada wa kulipa gharama zao za matibabu.

Mahakama katika uamuzi ilipiga kura saba dhidi ya mbili na kutupilia mbali juhudi za majimbo 18 yanayoongozwa na warepublican na utawala wa Rais wa zamani Donald Trump wa kubadilisha sharia ya huduma za afya ya bei nafuu ya mwaka 2010.

Ilikuwa mafanikio ya Rais wa zamani Barack Obama, ambapo Trump haraka aliikataa huduma hiyo inayojulikana kama Obamacare. Mahakama ya juu Marekani pia ilikataa changamoto kwenye sharia mwaka 2012 na maamuzi yote matatu yakiweka vifungu kama hivyo vya kisiasa kama vile kuwaruhusu vijana watu wazima kubaki kwenye sera za bima za wazazi wao hadi wanapofikisha miaka 26 na kuhakikisha inawahudumia wagonjwa wenye matatizo sugu ya afya.