Maambukizi ya HIV/Ukimwi kwa vijana yaongozeka Tanzania

Daktari nchini Tanzania atoa ushauri kwa mtu anaeishi na virusi vya HIV/Ukimwi.

Imeelezwa kwamba asilimia mbili ya maambukizi mapya ya virusi vya HIV/ Ukimwi nchini Tanzania yapo miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 na miaka 24

Your browser doesn’t support HTML5

HIV Tanzania


Mkutano wa vijana uliofanyika Jumanne Jijini Dar es-Saalam umebaini changamoto kubwa katika maambukizi mapya ya virusi hivyo vinakabili vijana.Tanzanai inakadiriwa kuwa na jumla ya vijana balehe 171,257 wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Dkt Fatima Mrisho ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kitaifa ya kudhibiti ukimwi,TACAIDS wakati Dkt Abdallah Posi ni Naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu wanaeleza hali halisi ilivyo.

Serikali imeeleza kwamba Miaka mitano ijayo inatoa fursa kubwa kwa Tanzania kuendeleza juhudi na kupanua utekelezaji wa mikakati ya kumaliza janga la HIV/Ukimwi ifikapo mwaka 2030,kwa kuwa maambukizi mapya ya yanaweza kuzuilika kwa kuwa na mikakati sahihi ya elimu na uhamasishaji hususan kwa vijana. Dinah Chahali anasimulia zaidi kutoka Dar es Saalam.