Akiwa katika madaraka kwa chini ya miaka mitatu, Rais wa 35 wa Marekani aliacha athari kubwa katika historia ya nchi hii na utamaduni wake.
Kaburi la Kennedy huko katika makaburi ya Arlington nje ya Jiji la Washington ni moja kati ya eneo lenye kuwavutia zaidi watalii. Inawavutia vijana ambao walikuwa hawajazaliwa wakati Kennedy alipouawa, na wengine katika zama zake.
James Thurber wa Kituo cha Tafiti za Bunge na Marais huko chuo kikuu cha American University anasema: “Nilikuwa niko chuoni wakati hilo linatokea. Kila mtu katika zama zetu alikuwa anajua wapi alipo wakati waliposikia msiba huo, na baadae kuona tukio lenyewe, ikiwa ni pamoja na maziko yake. Amerika iliduwaa na kuangalia hilo.”
Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa dunia nzima. Urais wa Kennedy ulikuja kujulikana kama Miaka ya Camelot, ambacho kikawa ni simulizi yake ambayo mkewe alisaidia kuitengeneza.
James Thurber anaendelea kusema kuwa : Kuna siri inayomzunguka na alikufa akiwa mdogo sana. Alikufa wakati watoto wake wadogo, na mke mrembo ambao wote walikuwa wanapendwa na Wamarekani.