Mmoja wa matajiri barani Asia, bilionea wa India, Gautam Adani, kwa mara nyingine ameingia kwenye vichwa vya habari duniani.
Hisa za kampunzi zake zimeshuka thamani kwa asilimia 20, Alhamisi baada ya kushitakiwa na waendesha mashitaka wa Marekani, kwa shutuma kwamba amewatapeli wawekezaji katika mradi mkubwa umeme wa nguvu za jua nchini India kwa madai kwamba umekuwa ukiendeshwa kwa rushwa.
Katika hati ya wazi ya mashitaka ya New York, Adani mwenye umri wa miaka 62, amefunguliwa mashitaka kwa kughushi masuala ya usalama na njama za kughushi masuala ya usalama wa mihamala ya mtandao.
Wakurugenzi wengine saba wenye uhusiano na himaya ya biashara ya Adani, pia wanakabiliwa na mashitaka.
Hati ya mashitaka inawashutumu kulipa takriban dola milioni265 za hongo kwa maafisa wa India.