Makamu wa rais wa Marekani, Kamala Harris, anahudhuria mkutano wa usalama wa Munich, ambapo anawahakikishia washirika wake ambao bado waendelee kuitegemea Marekani.
Katika hotuba yake fupi ya Ijumaa, makamu wa rais Harris, alitangaza habari za kifo cha kiongozi wa upinzani wa Russia, Alexey Navalny, na kusema kama ishara zaidi ya ukatili wa rais wa Russia, Vladimr Putin.
Aliomgeza kusema ni muhimu kwa maslahi ya watu wa Marekani, kwa taifa lake kuendelea na jukumu lake la muda mrefu la uongozi wa duniani.
Safari ya yake kwenye mkutano huo wa kila mwaka wa usalama inafanyika kukiwa na mashaka juu ya nafasi ya uongozi wa Marekani duniani wakati taifa hilo likikabiliwa na uchaguzi, huku mmoja wa wagombea, ni rais wa zamani Donald Trump, ambaye amedokeza ataihimiza Russia, kuwashambulia wanachama wa NATO ambao wamefanya uhalifu kwa kutotoa ada zao za NATO.