Wageni, wachezaji na mashabiki wa mpira wa miguu, wanaendelea kuwasili nchini Qatar, tayari kwa michuaao ya Kombe la Dunia mwaka 2022, ambayo itaanza rasmi kesho kutwa, na kwendelea hadi Desemba 18, wakati fainali itafanyika kwenye uwanja wa Lusail.
Tayari mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, Sunday shomari, amewasili mjini Doha, na atakuwa akiwajuza yanayojiri katika mashindano hayo ambayo yanakutanisha watu kutoka pembe zote duniani.
Hapa anaanza kwa kueleza hali ilivyo hasa baada ya habari kuibuka kwamba mchezaji nguli wa Senegal Sadio Mane hatashiriki katika michezo hiyo.
Your browser doesn’t support HTML5