Hakuna sherehe za Krisimasi Bethlehem

Kanisa la Nativity, Bethlehem. Desemba 24 2024

Mji mtakatifu wa Bethlehem, kwenye ukingo wa Magharibi umekosa shamra shamra za krisimasi kutokana na vita vya Gaza.

Bustan ya Manger umokosa mapambo yake ya kawaida sawa na kukosa watalii wanaotembelea sehemu hiyo wakati wa sherehe za krisimasi.

Kuna hali ya utulivu na kimya nje ya kanisa la Nativity lililojengwa mahali wakristo wanaamini kwamba ndipo alipozaliwa Yesu Kristo.

Vita na machafuko katika ukingo wa magharibi vimesababisha ukosefu wa kufanyika sherehe za krisimasi katika mji wa Bethlehem na hivyo kuathiri Uchumi wa mji huo, ambao kwa kiwasngo kikubwa mapato yake – karibu asilimia 70 - yanategemea utalii wa krisimasi.

Uchumi wa ukingo wa magharibi umeharibika sana kutokana na vizuizi dhidi ya wafanyakazi, ambao hawaruhusiwi kuingia Israel wakati huu wa vita.