Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa Jumatano imeeleza kwamba kuporomoka kwa haki za wanawake nchini Afghanistan.
Ripoti imeainisha kwamba imekuwa ni jambo la dhahiri kuonekana zaidi baada ya Taliban kuchukuwa utawala wan chi mwezi Agosti mwaka jana.
Tume ya usaidizi wa Afghanistan ya Umoja wa Mataifa ama UNAMA, imetoa ripoti katika mutano na wanahabari mjini Kabul, Jumatano.
Imesema imepata wasiwasi mkubwa kuhusu hali hiyo ya ukandamizwaji ambapo ukiukwaji wa waki za binadamu umekuwa ukifanyika mpaka leo.
Hali hii imetokea mara tu ya nchi kupatwa na mabadiliko ya Taliban kuchukuwa udhibiti wa nchi.
Ripoti hiyo imeeleza kwamba toka Agosti 15, wanawake na wasichana haki zao zimekuwa zikikiukwa hasa katika ushiriki wa elimu, sehemu za kazi na sehemu nyingine za umma, na maisha ya kila siku kuwekewa kanuni za kuwazuia ushiriki wao.