Watu hao jana Alhamisi walifika kituo kikuu cha polisi kuitikia wito wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa huo, Paul Makonda katika sakata linaloendelea la dawa za kulevya.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema timu maalum ya upelelezi iliyojumuisha vyombo vingine vya usalama inaendelea kuwahoji Manji na Mchungaji Gwajima.
Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ameripoti kuwa polisi imetangaza kuwatia mbaroni jana watu 11 pamoja na kete 38 za dawa za kulevya na magunia matano ya bangi.
Your browser doesn’t support HTML5
Aidha Kamanda Sirro amesema katika orodha ya watu 65 waliotakiwa hivi karibuni kuripoti kituo cha polisi ni wanne tu ndiyo waliojitokeza ambapo ametoa wito kwa wale wote waliotajwa katika orodha iliyotolewa juzi kujitokeza kwa hiari kabla jeshi hilo halijachukua hatua nyingine.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) leo katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma amesema hatakwenda polisi kuhojiwa kama alivyoamuru mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Mbowe hata hivyo amesema yuko tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika ikiwa taratibu sahihi zitafuatwa katika uchunguzi huo.
Your browser doesn’t support HTML5
Mbowe pia ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Bwana Makond kwa madai ya kumshushia hadhi kama mbunge na kiongozi wa upinzani bungeni kwa kumhusisha na tuhuma hizo za dawa za kulevya
Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Muungan wa Tanzania, John Magufuli, leo Februari 10, 2017 amemteua Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya (Drug Control and Enforcement Authority).
Imetayarishwa na Mwandishi wetu Dina Chahali, Tanzania