Alpha Conde aapishwa rasmi

Raia wa Guinea wakifurahia baada ya mahakama kuu nchini humo kumtangaza Alpha Conde mshindi

Guinea inapanga kumuapisha Rais wake mpya wakati nchi hiyo hatua itakayohamisha utawala wake kutoka wa kijeshi kwenda wa kiraia.

Rais mteule Alpha Conde anaapishwa Jumanne katika mji mkuu Conakry.Viongozi kadhaa wa Afrika akiwemo Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma, wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo za kiongozi mpya mwenye umri wa miaka 72.

Bwana Conde alishinda asilimia 52 ya kura katika duru ya marudio ya uchaguzi iliyofanyika Novemba, ambayo ilitambulika kuwa upigaji kura wa kwanza wa kidemokrasia nchini Guinea baada ya zaidi ya miongo mitano ya udiktekta na udhibiti wa kijeshi.

Duru ya marudio ya upigaji kura iliahirishwa mara nne kwa sababu ya mapigano ya mitaani, migogoro ya kisiasa na matatizo ya kiufundi, lakini waangalizi wa kimataifa walisema uchaguzi ulikwenda sawa.