Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, Alhamisi ametoa mwito wa dunia kuungana kwa ajili ya demokrasia na kukabiliana na ghasia za makundi ya msimamo mkali Afrika Magharibi, ambayo yamekuwa yakisambaa kusini kutoka Sahel kuelekea Ghana na majirani zake.
Rais Akufo-Addo, aliongea hayo mjini Washington, alipotaka msaada kama Ukraine, kutoka mataifa ya magharibi kupelekwa kwa nchi za kidemokrasia za Afrika magharibi, na kusisitiza kwamba madhara hayo ya ugaidi lazima yakabiliwe kwa pamoja.
Wakati wanamgambo wenye msimamo mkali wakidhibiti eneo kubwa la Mali, Burkina Faso, na Niger, Marekani na washirika wake wa magharibi wamekuwa wakiangazia kuisaidia Ghana, na mataifa mengine ya mwambao wa Afrika magharibi kuboresha ulinzi wao.
Wakati Ghana ikiwa bado haijakabiliwa moja kwa moja na ghasia za ugaidi, Togo, Benin, na Ivory Coast zote zimeshambuliwa na mashambulizi karibu na mipaka yake katika miaka ya karibuni.