Shirika moja lililoanzishwa na mcheza filamu wa Marekani George Clooney limesema limeungana na mtandao wa Google katika kutumia teknolojia ya satellite ili kufuatilia kwa karibu uwezekano wa uhalifu wa kivita kabla ya kura ya maoni ambayo inaweza kuigawa nchi hiyo katika nchi mbili.
Shirika hilo la Clooney kwa jina Not On Our Watch limesema juhudi hizo za kutumia mradi wa Satellite zitatoa mpango maalum wa onyo la mapema kabla ya kura ya maoni ya Sudan Kusini Januari 9 juu ya kujitenga na kuwa taifa huru au kubaki kama shemu ya Sudan.
Shirika hilo linasema litachukua picha za satellite ambazo zitaonyesha matembezi ya vikosi , raia na ishara nyingine endapo kutatokea mzozo kati ya upande wa kaskazini na kusini.