Gavana wa zamani wa Arkansas atangaza kugombea urais wa Marekani

Gavana wa zamani wa Arkansas, Asa Hutchinson ametangaza kugombea urais mwakani akijitolea kuwa mbadala wa Warepublican tayari kukigeuza chama hicho kutoka kwa Donald Trump.

“Nina uhakika kwamba watu wanataka viongozi wanaoitakia mema Marekani, sio wale wanaovutia hisia zao mbaya,” Hutchinson alikiambia kipindi cha This Week cha ABC katika mahojiano ya Jumapili.

Hutchinson, 72, aliondoka madarakani Januari baada ya miaka minane kama gavana. Amekuwa mkosoaji wa rais wa zamani Trump katika miezi ya hivi karibuni, akisema uteuzi mwingine wa Trump utakuwa mbaya zaidi kwa chama cha Republican na kunufaisha nafasi ya Rais Joe Biden mwakani 2024.

Hutchinson anajiunga na Balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Nikki Haley na mjasiriamali Vivek Ramaswamy, Gavana wa Florida Ron DeSantis, huku Seneta wa Marekani Tim Scott wa South Carolina na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo wakiwa miongoni mwa wanaofikiria kuwania urais.