Wanamgambo wanawatishia na kuwatia hofu wafanyakazi wa benki na wakati mwingine wanawateka nyara watoto wao na jamaa zao ili kuwalazimisha kwenda kazini, Kabir aliliambia gazeti hilo kwa njia ya simu.
Pia alisema majaribio ya Waziri Mkuu wa muda Abdulhamid al-Dbeibah kumuondoa kwenye nafasi yake yalikuwa kinyume cha sheria, na yalikiuka makubaliano ya mashauriano ya Umoja wa Mataifa juu ya udhibiti wa benki kuu.
Mgogoro wa udhibiti wa Benki Kuu ya Libya unasababisha kiwango kingine cha ukosefu wa utulivu katika nchi ambayo ni mzalishaji mkuu wa mafuta, taifa ambalo limegawanyika kati ya upande wa mashariki na magharibi ambazo zinapata uungwaji mkono kutoka Uturuki na Russia.