Gabon yasheherekea mwaka mmoja tangu mapinduzi ya kijeshi nchini humo

Serikali ya Gabon inaadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuondolewa madarakani kwa Rais Ali Bongo

Mwaka mmoja tangu mapinduzi ya kijeshi nchini Gabon yamalize utawala wa miaka 56 wa kiimla wa Rais Ali Bongo, nchi hiyo iliadhimisha kumbukumbu hiyo wiki hii kwa sherehe na ahadi za serikali ya kijeshi kuongeza kasi ya mchakato wa mageuzi.

Raia wa Gabon kwa kiasi kikubwa walikaribisha kuondolewa madarakani na jeshi kwa rais Bongo, ambaye usimamizi mbovu wa familia yake wa utajiri wa mafuta wa nchi hiyo ya Afrika ya kati ulipelekea uchumi kudorora na kukwama theluthi moja ya watu katika umaskini.

Mamia walikusanyika katikati mwa mji mkuu, Libreville, siku ya Ijumaa kwa ajili ya sherehe rasmi zilizoongozwa na rais wa mpito Jenerali Brice Oligui Nguema kuadhimisha mwaka wa kwanza wa kile kinachojulikana na wengi kama "mapinduzi ya ukombozi" nchini Gabon.