Your browser doesn’t support HTML5
Uwezekano wa kufanyika duru mpya ya mazungumzo ya Mashariki ya kati , umeanza vibaya, huku Israel ikikataa juhudi zozote za mazungumzo yasioyo ya moja kwa moja. Ufanransa inaandaa mkutano wa kimataifa wa mawaziri hapo Mei 30 katika juhudi za kufufua majadiliano ya amani ambayo ya mwisho yaloandaliwa na Marekani yalifanyika hapo mwaka 2014 . Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean Marc Ayrault alitembelea viongozi wa Israel na Palestina hio jana pale taifa lake linapojiandaa kufanya mkutano wa kimataifa wa amani unaolenga kutafuta njia za kufufua mazungumzo ya amani.
Wapalestina jumapili waliadhimisha kile walichokiita “siku ya janga” inayoaadhimisha siku maelfu a wapalestina walipopoteza makazi yao kufwatia kubuniwa kwa taifa la Israel . Maandamano yalifanyika katika maeneo yote ya palestina, siku moja baada ya Israel kuadhimisha miaka 68 ya uhuru wake.
Huko mjini Bethlehem, washiriki walipanda magari moshi yaliyoandikwa miji ya zamani ya vijiji vya Palestine. Waandaaji wanamatumaini ya kurejea vijiji hivyo.
Wanajeshi wa Israel waliwarushia gesi ya kutowa machozi waandamanaji kwenye kizuizi huko Ukanda wa magharibi, na baadhi ya wapalestina huko Gaza walirusha mawe kwenye uzio na Israel.
Hii ndio hali waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean Marc Ayrault alikumbana nayo wakati wa ziara yake katika mjii mkuu wa ukanda wa magharibi Ramallah jana, alipokuwa na mkutano na rais wa palestina Mahmoud Abbass.
Lakini Israel bado inalaumu kuwa azimio la idara ya umoja mataifa ya UNESCO mwezi ulopita lilolaani Israel kwa ukaliaji wa kimabavu msikiti wa Al Aqsa, na hivyo kuwanyima waislamu uhuru wa kuabudu. Eneo hilo linaheshimiwa na wote wayahudi ambalo wanaliita Temple Mount na ni mojawapo ya maeneo matakatifu katika Imani ya Judea.