Rais wa Finland, Sauli Niinisto, Jumanne amesema kuvuja gesi kuliko sababisha kufungwa kwa bomba la gesi asilia kutoka Estonia, hadi Finland, mwishoni mwa juma huenda kulisabishwa na shughuli za nje.
Mwaka jana, kulikuwa na mfululizo wa milipuko ya chini ya maji ambayo ilipasua mabomba matatu ya gesi asilia kutoka Russia, mpaka Ulaya magharibi wakati wa mvutano mkubwa wa siasa za kikanda ulipozidi ambapo Moscow, ilisimamisha usambazaji wa gesi kwenda Ulaya.
Wakati serikali ikionya kufikia hitimisho lolote, inasema inaonekana si vilipuzi ndio vimesababisha, imesema taasisi ya NORSAR ya Norway, kuwa Jumatatu iligundua mlipuko katika eneo la linakovu.
Rais Niinisto, amesema amekuwa akiwasiliana na katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, na kwamba muungano huo wa kijeshi upo tayari kusaidia uchunguzi wake.