Aliyeua watu 50 Florida atajwa kama Omar Mateen

Gay club shooting

Na BMJ Muriithi

Polisi katika mji wa Olarndo, jimbo la Florida, nchini Marekani, wametoa jina la mtu aliyeshambulia klabu cha usiku mjini Orlando, Florida, na kuua takriban watu 50 na kujeruhi 53 kama Omar Mateen ambaye ni raia wa Marekani.

Polisi wamethibitisha kuwa msshukiwa huyo, ambaye alivamia bar maarufu kwa watu wa mapenzi ya jinsia mooja iitwayo Paulse, alikuwa na bunduki mbili, na aliwashika watu mateka na kufyatuliana risasi na polisi kabla ya kuuawa.

Kulingana na taarifa kutoka kwa polisi, mshukiwa huyo aliingia kwenye kilabu hicho muda mfupi tu baada ya saa nane usiku wa kuamkia Jumapili na kuanza kufyatua risasi kiholela.

Walinda usalama walikabiliana naye kabla ya kuitisha msaada kutoka kwa wenzao ambao walifika na kuingia kwenye jengo hilo na kuendelea kukabiliana na mtu huyo.

Msemaji wa polisi amewaambia waandishi wa habari kuwa wanalichukulia shambulizi hilo kuwa la kigaidi.

Shambulizi hili limetajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea Marekani tangu shambulizi la Septemba 11, 2000.

Wengi wa majeruhi walikimbizwa hospitalini ambako wanaendelea kupata matibabu.