Takriban watu 83 wamefariki dunia Alhamisi baada ya feri walimokuwa wakisafiria kupinduka kwenye mto Tigris karibu na mji wa Mosul nchini Iraq.
Maafisa wa serikali walisema kuwa zaidi ya watu 180 walikuwa kwenye kivuko hicho wakisherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa Kikurdi pamoja na ile ya Mother’s Day.
Walieleza kwamba wengi wa waathirika ni wanawake na watoto ambao walionekana wakijaribu kuogelea kwenye mto huo ambao maji yake yalikuwa na kasi kubwa.
Mmoja wa waokoaji, Abdul-Razak Falih aliiambia Sauti ya Amerika alhamisi kwamba aliopoa miili 20 kutoka majini na kwamba idadi ya waliokufa inatarajiwa kuongezeka.
Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad ulituma salam za rambirambi kwa jamaa za wahanga wa ajali hiyo.