FBI ina mashaka na programu ya ujasusi ya China

Mkurugenzi wa FBI, Christopher Wray akizungumza katika komngamano la dunia la uchumi, Davos, Uswisi, Januari. 19, 2023.

Mkurugenzi wa idara ya upelelezi ya Marekani FBI, Christopher Wray, Alhamisi amesema kwamba ana mashaka makubwa na programu ya kijasusi ya serikali ya China, akisisitiza haija tengenezwa kwa kufuata utawala wa sheria.

Akizungumza wakati wa kikao katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos, Uswizi, Wray alisema matarajio ya Beijing ya teknolojia ya kuendesha mambo maarufu kama AI ilitengenezwa kwa misingi mikubwa ya wizi wa ubuniafu wa teknolojia.

Vilevile ilizingatia uchukuliwaji wa taarifa nyeti na unyanyasaji ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa bila kudhibitiwa, China inaweza kutumia maendeleo ya kijasusi kuendeleza shughuli zake za udukuzi, wizi wa hati miliki na ubunifu pamoja na ukandamizaji wa wapinzani ndani ya nchi na kwingineko.