Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, anyajulikana sana kama Farmajo, amewaonya wanasiasa kuacha kuchukua hatua ambazo zinaweza kuhujumu usalama wa uchaguzi wa bunge, unaonedelea.
Farmajo amehimiza viongozi wa Somalia kuangazia kabisa namna ya kukamilisha uchaguzi huo na kusuluhisha migogoro kupitia kwa njia ya mazungumzo.
Matamshi yake yametolewa saa chache baada ya waziri mkuu Mohamed Roble, kuamurisha mjumbe maalum wa umoja wa Afrika Frnacisco Madeira kuondoka Somalia ndani ya kipindi cha saa 48.
Rais Farmajo amepingas uwamuzi huo, ofisi yake ikisema kwamba haijapokea ripoti zozote za uhuru wa Somalia kuingiliwa na haungi mkono hatua isiyo halali dhidi ya Madeira.