Tuhuma hizo kwenye video zimetolewa baada ya mamake Alexei, Lyudmila kusema kuwa amezuiliwa kuuona mwili wake kwa siku ya tatu mfululizo, wakati ikulu ya Kremlin ikisema uchunguzi kutokana na kifo chake unaendelea.
Kifo cha Navalny akiwa kwenye gereza moja ya Russia wiki iliopita kimeshtua viongozi wa upinzani wa Russia waliokimbilia mataifa ya kigeni, pamoja na mataifa ya magharibi, wakati kidole cha lawama kikielekezwa kwa Kremlin.
Yulia Navalny Jumatatu amekutana na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Charles Michel mjini Brussels, baada ya kutoa tuhuma zake dhidi ya Putin na baada ya waziri wa mambo ya nje wa Ujeruimani Annalena Baebock, kusema kwamba atapendekeza vikwazo vipya dhidi ya Moscow kutokana na kifo cha Navalny