Familia ya Aysenur inataka uchunguzi huru kuhusu kifo chake huko Ukingo wa Magharibi

Wapalestina waandamana kutoa heshima zao kwa mwanaharakati Mmarekani mwenye asili ya Uturuki Aysenur Ezgi Eygi, huko Nablus, ukingo wa Magharibi

Familia ya mwanaharakati M-marekani mwenye asili ya Uturuki aliyepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano dhidi ya makazi ya walowezi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi imetaka uchunguzi huru ufanyike kuhusu kifo chake, ikilishutumu jeshi la Israel kwa kumuua “kikatili”.

Aysenur Ezgi Eygi mwenye miaka 26, alipigwa risasi kichwani wakati akishiriki katika maandamano huko Beita katika Ukingo wa Magharibi siku ya Ijumaa.

“Uwepo wake katika maisha yetu ulichukuliwa bila ya sababu, kinyume cha sheria, na kwa nguvu, za jeshi la Israeli,” familia ya Eygi ilisema katika taarifa. Raia huyo wa Marekani, Aysenur, alikuwa kwenye maandamano ya amani akitafuta haki, wakati alipouawa kwa risasi ambapo video inaonyesha ilitoka kwa jeshi la Israeli.

“Tunatoa wito kwa Rais Joe Biden, Makamu wa Rais Kamala Harris, na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, kuagiza uchunguzi huru juu ya mauaji ya raia wa Marekani yaliyofanywa kinyume cha sheria, na kuhakikisha uwajibikaji kamili kwa wale wanaokutwa na hatia.