Facebook yatuhumiwa kufanya makubaliano ya siri bila ya kuwashauri wateja wake

FILE - Facebook's founder and CEO Mark Zuckerberg meets with French President Emmanuel Macron at the Elysee Palace after the "Tech for Good" summit, in Paris, France, May 23, 2018.

Facebook imetuhumiwa kufanya makubaliano ya siri na wanaotengeneza app zinazotumika katika mitandao ya kijamii ikiwaruhusu kutumia taarifa za watumiaji wa mtandao huo na kudukua simu na kompyuta zao kuingilia taarifa za watu wengine nje ya mtandao wa Facebook.

Mbunge Danian Collins ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Idara ya Digitali, Utamaduni, Mitandao ya Kijamii na Mchezo ya Uingereza ameleza wasiwasi wake juu ya mambo kadhaa yanayohusu kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii.

Inadaiwa kuwa Facebook iliruhusu baadhi ya makampuni kuwa na uwezo zaidi wa kufikia orodha za marafiki wa wateja wa Facebook baada ya kubadilisha kanuni zake mwaka 2015.

Pia linalo tiliwa mashaka ni ukusanyaji wa taarifa za watumiaji unaofanywa na Facebook kwa watumiaji wa vifaa vya Android, ambako ilikuwa imeweka rekodi ya number za simu zilizokuwa zimepigwa na ujumbe uliokuwa umetumwa kwa kuiwezesha kampuni hiyo kutoa mapendekezo yao kwa watumiaji ni namba gani za mawasiliano ziwekwe mwanzoni katika app ya messenger.

Kampuni hiyo pia imetajwa kuwa ilitumia kampuni nyingine inayoitwa Onavo kuzifuatilia apps zilizokuwa zimewekwa katika simu.

Kwa mujibu wa repoti hiyo, lengo lilikuwa kutafuta apps ambazo zinashindana na Facebook au kuzinunua zile ambazo zinaweza kuwa muhimu kwa matumizi ya Facebook.

Kamati hiyo pia imetaja kuwa katika kubadilishana barua pepe, mtendaji wa ngazi ya juu Justin Osofsk na Mark Zuckerberg walijadili safu ya Twitter inayohusika na uchapishaji wa picha za video, Vine.

Huduma hiyo ilikuwa inatumia Facebook kuwasaidia watumiaji kutafuta marafiki kuwafuatilia na kuwakaribisha. Katika mawasiliano hayo Osofsk alipendekeza kuondoa uwezekano wa Twitter kuwafikia akaunti za marafiki wa Facebook.

Zuckeberg alikubali wazo hilo. Vine katika siku za baadae ilikuja kufeli kufanya hivyo, lakini haiko wazi iwapo hatua ya Facebook iliathiri kwa namna yoyote hilo.

Facebook imeeleza hisia zake katika taarifa yake ikiwa na hasira, na kuweka tamko lake juu ya nyaraka hizo na kueleza msimamo wake kwa kila nukta.

Kampuni hiyo imekanusha vikali madai mengi yaliyokuwa yametolewa. Ilikuwa inajikita kwa nguvu zote kujitetea juu ya suala la kusambaza taarifa za marafiki wa ziada kwa baadhi ya wanaotengeneza apps na kutowapa wengine.

Kampuni hiyo imesema kuwa hatua hii ilikuwa kwa ajili ya kuwasaidia watengenezaji hao kuhamisha apps zao kwa kufuata kanuni mpya ili kuzuia matatizo.

Facebook imesema kuwa wateja wake walikuwa wamepewa fursa ya kuamuwa kukubali au kukataa taarifa zao za namba za simu au ujumbe wa maandishi kutumika. Imesema kuwa hili lilihitajika kujadidi taarifa hizo kila mara kwa sababu taarifa zilizopitwa na wakati hazina matumizi yoyote kwa ajili ya kutathmini watumiaji wake wake wanaotumia app ya messenger.