Jumuiya ya ulaya imesema Jumatano kwamba itaongeza msaada zaidi katika ujumbe wa kijeshi Afrika nchini Msumbiji wakati mashambulizi ya Waislamu wenye msimamo mkali yakitishia miradi ya gesi yenye lengo la kupunguza utegemezi wa nishati kutoka Russia.
EU inatafuta njia nyingine mbadala ya nishati tangu Moscow ilipovamia Ukraine na Msumbiji ina hifadhi ya tatu kwa ukubwa Afrika.
Katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika limekuwa likishambuliwa na wanamgambo wanaohusiana na mtandao wa Islamic State katika jimbo lake lenye utajiri mkubwa wa gesi – Cabo Delgado tangu mwaka 2017.
Mzozo huo uko karibu na miradi ya gesi asilia LNG yenye thamani ya mabilioni ya dola iliyotengenezwa na makampuni ya magharibi ikiwa ni pamoja na Total ya ufaransa. Ikithibitisha taarifa ya Reuters ya mwezi Agosti EU serikali zimethibitisha kutoka dola milioni 15 katika ujumbe wa Jumuiya ya SADC kwa ajili ya msumbinji SAMIM ambao unapambana na uasi nchini humo.
Katika ripoti ya ndani iliyoonekana na Reuters Jumuiya ya ulaya ilionya juu ya hali tete kaskazini mwa msumbiji licha ya ujumbe wa SADC na uingiliaji tofauti wa vikosi kutoka Rwanda vinavyoweza kudhibiti wanamgambo.