Kufuatia tukio hilo la Jumapili, tayari mashirika kadhaa ya ndege yakiwemo yale ya Ufaransa,Lufthansa na Singapore yamesema kuwa hayatarusha ndege zao kwenye anga ya Belarus.
EU pia inachunguza tukio hilo wakati ikitadhmini kuhusu hatua itakazochukua dhidi ya maafisa wa Belarus waliyo amuru hatua hiyo ichukuliwe.
Tayari kuna maafisa kadhaa kutoka serikali ya Belarus waliowekewa vikwazo na EU kutokana na kuhusika kwenye msako wa mwaka jana baada ya uchaguzi wa rais uliozua utata.
EU pamoja na Marekani wameomba serikali ya Lukashenko kumuachilia mara moja Raman Pratasevich ambaye ni blogger mwenye umri wa miaka 26 na ambaye amekuwa akiishi uhamishoni nchini Poland.
Mtayarishaji - Harrison Kamau